

Lugha Nyingine
2月MPV:同环比继续双降 自主品牌包揽前三
Soko la Xicang katika Eneo la Lianhu la Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China hapo awali lilikuwa sehemu ya ghala la nafaka la China wakati wa Enzi za Ming na Qing ya nchi hiyo ya zama za kale, na sasa hujaa hali moto moto ya maisha kila Alhamisi na Jumapili. Gulio hilo lenye historia ya miaka 100 limepitia hali mbalimbali na kuwa moja ya vituo vikubwa zaidi vya biashara ya mitumba vya ngazi ya chini, vilevile ni alama hai ya mila na desturi za jadi za wenyeji.
Tangu mwaka 2024, maeneo hayo yamekuwa yakipitia juhudi za kuhuisha miji ili kusaidia kuhifadhi soko hilo la jadi katika msingi wake wakati huohuo kuboresha miundombinu iliyopo, na kujenga upya Bustani ya Kumbukumbu za Mji ya Xicang. Mkakati huo umeruhusu mitindo ya kisasa ya vijana kuishi pamoja na mvuto wa kipekee wa soko, ikiingiza hali mpya moto moto kwenye eneo hilo la kihistoria.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma