

Lugha Nyingine
蓁是什么意思
SHANGHAI - Kampuni vumbuzi ya kiteknolojia ya China imewasilisha kwa mteja ndege ya kiwango cha tani ya kupaa na kutua wima (eVTOL) jana Jumanne, ikimaanisha mafanikio mapya katika matumizi ya eVTOL kubwa, ambapo ikiwa imeundwa na kampuni ya Shanghai ya AutoFlight, ndege hiyo ya V2000CG CarryAll ina uzito wa juu wa kupaa wa tani 2.
Kufuatia upataji wa cheti cha muundo wake na cheti cha uzalishaji mwaka jana, pamoja na cheti cha kustahiki kuruka angani kilichopatikana siku ya Jumatatu wiki hii, ndege hiyo inayojiendesha bila rubani itakuwa ikiendeshwa na kampuni ya biashara ya usafiri wa anga ya chini yenye makao yake Guangzhou.
V2000CG CarryAll ina uwezo wa kupakia wa hadi kilo 400 na kasi ya juu ya kusafiri ya kilomita 200 kwa saa na kusafiri masafa ya kilomita 200. Ina uwezo wa kupaa na kutua wima na muundo wa kuzunguka kwa mabawa yasiyobadilika, ikiwezesha matumizi yake katika uchukuzi wa anga ya chini, mwitikio wa dharura na nyanja zingine.
Xie Jia, naibu mkuu mwandamizi wa AutoFlight, amesema kuwa aina hiyo ya ndege hadi sasa imekamilisha kilomita zaidi ya 40,000 za safari salama katika maeneo mbalimbali ya China na nchi nyingine kama vile Falme za Kiarabu na Japan, ambayo inasaidia kuthibitisha ufanisi wake na kuchunguza mazingira ya uwezekano wa matumizi yake.
Uwasilishaji huo wa eVTOL unakuja wakati uchumi wa anga ya chini wa China unaingia katika hatua ya ukuaji wa haraka ambapo kwa mujibu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya China, thamani ya soko la sekta hiyo itapanda kutoka yuan bilioni 500 (dola za Kimarekani kama bilioni 70) mwaka 2023 hadi yuan trilioni 1.5 mwaka 2025, na kiasi hicho kinaweza kufikia yuan trilioni 3.5 ifikapo mwaka 2035.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma